Diamond atikisa tuzo za Kilimanjaro Music Award 2013-14


Diamond na mpenzi wake Wema Sepetu wakiwa katika furaha jana nje ya ukumbi wa Mlimani city baada kunyakua tuzo 6 za kill

Hatimaye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo  za Kilimanjaro Tanzania Music Award [KTMA] kilifikia tamati hapo jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa kuwatunuku wasanii,makundi bora kwa aina zote za muziki na watayarishaji bora wa nyimbo kwa mwaka wa 2013-2014.

Katika tuzo hizo msanii machachari wa kizazi kipya nchini Diamond ameweza kuvunja rekodi kwa kuibuka kidedea kwa zaidi ya tuzo 6 kwa vipengele tofaut i alivyoshiriki ikiwemo mtunzi bora wimbo wa kizazi kipya,mtumbuizaji bora wa kiume,video bora ya mwaka kwa wimbo wa my number one,muziki bora wa mwaka,muimbaji bora wa kiume wa kizazi kipya na  wimbo bora wa Afro pop.

Waliofuatia kwa tuzo zaidi ya moja ni Mzee Yusuf kwa tuzo  nne ikiwemo moja kundi bora la muziki wa Taarabu,Mashujaa band tuzo mbili kwa kuwa bendi bora ya mwaka na wimbo bora wa bendi wa mwaka wa Kiswahili,Fid Q amepata tuzo ya mtunzi bora wa Hiphop na msanii bora wa Hiphop,Lady Jaydee amepata tuzo ya wimbo bora wa Zhouk na mwimbaji bora wa kike wa kizazi kipya.

Walioambulia tuzo mojamoja ni Chibwa akiwa mtunzi bora wa Rege,wimbo bora wa rege ni DOUBLE BOO,muziki wenye vionjo vya asili ni Da Bongo massive,Young Killer ni msanii bora chipukizi,Christian Bella ni mtunzi bora wa kizazi kipya katika bendi,Enrico ni mtayarishaji bora wa nyimbo za taarabu,Amorosso ni mtayarishaji bora wa nyimbo katika bendi,Niki wa 2 nyimbo bora ya mwaka ya hiphop[nje ya box],Ney wa mitego na Diamond ni wimbo bora wa kushirikiana [muziki gani],Jose Chamelion ni wimbo bora wa Afrika Mashariki [tubonge],Man Walter ni mtayarishaji bora wa muziki wa kizazi kipya,Hassan Bitchuka amepata tuzo ya heshima,Isha Ramadhanii ni mtumbuizaji bora wa kike,Ferguson ni rapa bora katika bendi,kikundi bora cha mwaka kizazi kipya ni Weusi,wimbo bora wa RnB ni wa Vanessa Mdee[crazy] na muimbaji bora wa kike katika bendi ni Luiza Mbutu.

Tuzo za Kilimanjaro Music Award hufanyika kila mwaka kwa lengo la kukuza na kuongeza ufanisi na hamasa kwa wasanii,watunzi na watayarishaji wa muziki ili kuhakikisha unasonga mbele hapa ambapo mwaka huu kulikuwa na vipengele vipatavyo 36 vilivyoshindaniwa vilivyowafanya wasanii walichopanda na kukivuna huku Diamond akiwa gumzo kwa kubeba tuzo sita.

Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

Post a Comment

 
Top