SIASA YA TANZANIA NA MWENDO WA KUTOANA VIBANZI
SIASA YA TANZANIA NA MWENDO WA KUTOANA VIBANZI
NA ANDWELE MWAMBENE-0763077688
Ukweli na uwazi ni jambo la muhimu na msingi sana katika jamii huru inayojitambua katika kulisukuma gurudumu la maendeleo.Huu usemi umewahi kunukuliwa pia toka kwa Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa aliyekuwa akipendelea kusema kuwa huu ni wakati wa ukweli na uwazi ingawa wengi waliona msemo huo kama ni nadharia tu pasipo kujua uzito uliomo ndani yake.
Jamiinyingi duniani zimekuwa zikipiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kasi na kwa ufanisi mkubwa kutokana na suala zima la kuambiana ukweli pale wanapoona pamepotoka na wahusika kuwajibishwa kulingana na walichokifanya na ni kwa kiasi gani.
Nikianzia moja kwa moja na mada niliyokuandalia katika makala haya kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye mifumo ya sia ya vyama vingi [kidemokrasia] na isiyo na dosari yoyote yenye mantikiya umwagaji damu kutokana na siasa ukilinganisha na nchi nyingine zinazotuzunguka zilizowahi ukmwaga damu na zinazoendelea kumwaga damu ambazo ni Rwanda,Burundi,Jamhujri ya kidemokrasia ya kongo,Somalia na Sudani,bali ni sisi pekee ambao ni mfano wa kuigwa kwa hilo ingawa kuna baadhi wasioitakia mema nchi yetu.
Mfumo wa vyama vingi Tanzania ulirasmishwa mnamo mwaka 1992 toka mfumo wa chama kimoja na kuruhusu demokrasia ya vyama vingi ili kuleta chachu ya maendeleo kwa kushauri na kukosoa makosa ya chama kinachokuwa madarakani kwa ajili ya manufaa ya umma ingawa kwa sasa wengi hukosoa kwa manufaa binafsi ya kuchafuana na kujitengenezea mazingiira ya
kushika hatamu ya uongozi kwa mapinduzi ya fikra,,lakini kwa upande wa mazuri wamekuwa wazito kutoa pongezi kwa watawala.
Siasa ya Tanzania kwa siku ya hivi karibuni inaelekea kuchuja na kupoteza uhalisia kwa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo kutupiana vijembe kati ya chama na chama na wenyewe kwa wenyewe ndani ya vyama husika na kusahau kwa yale wanayowatupia lawama na wao pia kuanza kuyarudia yale yale.
Tukianzia katika chama tawala yaani Chama cha Mapinduzi [CCM] kumekuwa na hali ya kuoneana aibu kuambiana ukweli kwa viongozi wanaokwenda kinyume na maadili hasa katika masuala yanayowahusu wananchi.Masuala ya KIFISADI yanaishia tu katika adhabu za midomoni na kujivua gamba na baada ya hapo mambo huishia kimyakimya jambo ambalo hufanya wananchi kuanza kujiuliza kulikoni.Kuna maswali mengi kuwa ni kwa nini hakuna hatua zozote hazichukuliwi au ndio kusema samaki mmoja akioza inamaanisha wote wameoza?
Ninavyojua ni kwamba dhamana ya chama kinachokuwa madarakani ni kuhakikisha kinasimamia haki na usawa kwa wananchi wake badala ya kuleta udugu na urafiki na kusababisha kushindwa kutekeleza ahadi kwa wananchi waliowapa dhamana hiyo .Lakini jambo la kushangaza pindi nyakati za uchaguzi zinapokaribia hekeheka huwa nyingi kama ni Mbunge ndio kipindi cha kurudi jimboni kuwarubuni wananchi wakati tangu waliposhika hatamu badhi ya Wabunge majimbo yao huwa yatima kwa kipindi cha nusu mlongo kwani shida zao ni madaraka tu.
Halikadharika kwa upande wa vyama pinzani tabia hazipishani sana na chama tawala bali tofauti ni kwamba hatuna uzoefu sana na vyama hivyo kushika hatamu ya nyadhifa za ngazi za juu ila husaidia kuleta changamoto kwa chama kilichopo madarakani kuwa makini kwa kuogopa kuangushwa katika chaguzi mbalimbali nchini na kwamba si nadharia baadhi ya chaguzi chama tawala kimeweza kupokwa na wapinzani mfano Arusha Chadema imeweza kushinda viti kadhaa vya madiwani.
Hivi karibuni tumeona mvurugano uliojitokeza katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] kati ya aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe nachama kwa kile kilichodaiwa kupanga njama za kutaka kukihujumu chama hicho.
Lakini cha kushangaza pia ni kuona kuwa mbona hatua hiyo ya kumwadhibu Zitto ilikuja mara baada ya kuanza kuvibana vyama vyote vya vinavyopewa ruzuku na Serikali kikiwemo CHADEMA kuwasilisha mapato na matumizi ya fedha hizo?
Hayo pia yalidhihirika hivi karibuni katikt mchakato wa Bunge maalum la katiba kwa kuacha kujadili rasimu ya katiba ya wananchi na kuanza kutupiana vijembe na kuwasahau walipa kodi wakiumia maana waliotumwa kuwatetea wanaacha majukumu yao na kuangalia maslahhi yao binafsi ambapo baadhi yao walithubutu kutoka bungeni kwa kuacha kuwatetea wananchi kwa hoja na kudai wanarudi kwa wananchi.
Nimalizie makala haya kwa kusema ni wakati wa vyama vya siasa nchini kubadilika kwa kutokutoa vibanzi kwa wengine kabla ya kuanza kujisafisha kwanza wenyewe maana wameamua kuingia katika siasa kwa lengo linalofahamika la kutetea haki na maslahi ya wananchi.Lakini kwa upande mwingine sitosita kuwapongeza kutokana na changamoto mbalimbali walizozitoa kwa Serikali kwa lengo la kuboresha maisha ya Mtanzania wa kawaida.
Post a Comment