Image copyrightepa
Image captionPapa Francis
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amewasili kisiwa cha Lesbos kuonyesha kuwaunga mkono wakimbizi wanaojaribu kufika barani Ulaya.
Papa Francis ameandamana na kiongozi wa kanisa la Orthodox Bartholomeo Constantinople.
Wawili hao watatembelea kambi iliyo kisiwani humo, ambapo wahamiaji zaidi ya 3,000 wanazuiliwa, wakisubiri kusafirishwa kwenda Uturuki chini ya makubaliano ya muungano wa ulaya.
Papa amesema safari yake Ugiriki ni ya kwenda kushuhudia mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu tangu kumalizika kwa vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Makubaliano hayo yamekosolewa na mashirika ya kutoa misaada na makundi ya kutetea haki za binadamu.
Vatican imesema ziara hiyo ya Papa ni ya kibinadamu na kidini na haifai kutazamwa kwa vyovyote vile kama ukosoaji wake wa mpango wa kuwatoa wahamiaji Ugiriki na kuwapeleka Uturuki.

Post a Comment

 
Top