BrazilImage copyrightAP
Image captionWatoto wengi wamekuwa wakizaliwa wakiwa na vichwa vidogo Brazil
Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Magonjwa Marekani (CDC) kimethibitisha kwamba virusi vya Zika husababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo na ubongo kudumaa.
Kumekuwa na mjadala mkubwa na suitafahamu kuhusu uhusiano kati ya virusi hivyo na watoto kuzaliwa na vichwa vidogo tangu kuongezeka kwa visa vya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Brazil.
Mkurugenzi mkuu wa CDC Tom Frieden amesema hakuna shaka kwamba virusi vya Zika vinasababisha watoto kuzalwia na vichwa vidogo, tatizo ambalo kwa Kiingereza hujulikana kama microcephaly.
Maafisa wa CDC wamesema kwamba bado wanawashauri wanawake wajawazito kutozuru maeneo ya Amerika Kusini na visiwa vya Caribbean, ambako maambukizi ya virusi hivyo yameripotiwa.
Virusi vya Zika huenezwa sana na mbu ingawa kumeripotiwa pia visa vya watu kuambukizwa virusi hivyo kupitia kufanya mapenzi.
Kumeripotiwa visa 346 vya maambukizi ya virusi hivyo Marekani.
Jumatatu, maafisa nchini humo walionya kwamba mlipuko wa sasa wa virusi vya Zika huenda ukaathiri sana Marekani na wakaomba kutolewe ufadhili zaidi.
"Kila kitu tunachofahamu kuhusu virusi hivi kinaonekana kuwa cha kuogofya zaidi ya tulivyodhania," alisema Dkt Anne Schuchat kutoka CDC.
ZikaImage copyright
Image captionVirusi vya Zika huenezwa sana na mbu
Virusi vya Zika viligunduliwa mara ya kwanza mwaka 1947 nchini Uganda, lakini dalili za kuambukizwa virusi hivyo hazijakuwa kali. Wengi wa wanaoambukizwa walikuwa wakipatwa na homa ambayo si kali sana, mwasho na maumivu katika maungio.
Mlipuko wa sasa ulianza mwishoni mwa mwaka 2015 nchini Brazil na dalili zake zimekuwa kali.
Watoto karibu 200 wamefariki kutokana na virusi hivyo.


Post a Comment

 
Top