Tanzania
Tanzania

 NDUGU WATANZANIA NCHI YETU IMEFIKA MAHALI AMBAPO TUNAPASWA KUMSHUKURU MUNGU KUTOKANA NA AMANI TULIYONAYO KWA KIPINDI CHA TAKRIBANI MIAKA HAMSINI TANGU KUPATA UHURU TOKA MIKONONI MWA WAKOLONI.

PAMOJA NA HAYO JAMBO LA KUSHANGAZA NI PALE TUNAPOONA BAADHI YA WATU WASIOITAKIA MEMA NCHI YETU KWA KUANZA KUTOA MANENO AMBAYO YANAWEZA KUIPOTEZA NCHI YETU KATIKA RAMANI YA NCHI CHACHE DUNIANI ZILIZOBAHATIKA KUUNGANISHA WATU WAKE NA KUWA KITU KIMOJA.

MASIKITIKO YANGU MAKUBWA NI KWA WANASIASA AMBAO NDIO DIRA YA NCHI KATIKA MASUALA MBALIMBALI IKIWEMO KUHAKIKISHA DEMOKRASIA INADUMISHWA,AMANI NA UPENDO ILA CHA AJABU NI KUONA WANAKUA CHACHU YA KUCHOCHEA CHUKI MIONGONI MWA WANANCHI KWA MASLAHI YAO BINAFSI.

SINA MENGI YA KUZUNGUMZA KWA LEO ILA NI KUWAHUSIA WATANZANIA WENZANGU KUWA TUOGOPE YALE MABAYA YENYE LENGO LA KUHARIBU AMANI YETU ILIYODUMU ENZI NA ENZI NA KUWA KIMBILIO KWA NCHI ZILIZOKUMBWA NA MACHAFUKO YA KISIASA.

Post a Comment

 
Top