ZOEZI LA UHAKIKI KADI ZA YANGA TAWI LA YOMBO VITUKA
Zoezi la uhakiki kadi linaanza mwanzoni mwa mwezi huu mei , pia wale ambao kadi zao zina matatizo wanatakiwa wafike ofisini mapema kwa ajili ya kutatua matatizo yao.
Akizungumza na ANDWELE BLOG , katibu wa tawi hilo na afisa habari wa tawi ndugu Yusuph mwamba, alisema zoezi hilo ni muhimusana kwa wanachan,a wa tawi hilo ili kuweza kubaini matatizo ya kadi zao na kuzilekebisha ikiwemo kuwasisitizia wanachama kulipia kadi zao ukizingatia na ujio wa uchaguzi na kuwapa wanachama fulsa na haki ya kikatiba katika mchakato wa uchaguzi juni 6.
Aidha katibu alisisitizia kwamba miongoni mwa mambo yatakayofanyiwa uhakiki ni makazi ya mwanachama, namba ya simu na wakaribu yake,namba ya kadi pamoja na reja, malipo ya kadi pamoja na zoezi la kujaza fomu kwa wanachama wapya.
Hata hivyo pamoja na katibu kuzungumza hayo , pia Mwenyekiti wa tawi hilo ndugu Kassim abdallah kobichi naye amesisitizia swala la michango kwa wanachama walipe kwa wakati ili kuendesha shughuli za tawi na malipo ya ofisi.
Post a Comment