Historia
Kihistoria watu wanaoitwa leo Wanyakyusa waliitwa Wakonde, ambao kati yao Wanyakyusa walikuwa ndio kabila kubwa. Wakati wa karne ya 20 "Wanyakyusa" limekuwa jina la kundi kwa jumla.
Hadi leo kanisa la Kilutheri la KKKT linatumia jina "dayosisi ya Konde" kwa eneo lake katika mkoa wa Mbeya.
Wakati Wajerumani walipofika sehemu za kaskazini kwa Ziwa Nyasa mwisho wa karne ya 19 hawakuona tofauti ya kimsingi kati ya watu wa Malawi kaskazini na wale wa sehemu za Rungwe wakawaita wote "Wakonde" kutokana na jina lililokuwa kawaida ziwani.
Mgawanyiko wa Wanyakyusa
Wanyakyusa toka zamani walijulikana kama watu wa Konde. Wengi walikuwa kaskazini kwa ziwa Nyasa, lakini katika harakati za maisha na mabadiliko ya mazingira wengi wao wakakimbilia Mbeya mjini na sehemu nyingine.
Pamoja na hayo, hasa Wanyakyusa wapo wa aina mbili nao ni Wanyakyusa wa Tukuyu na Wanyakyusa wa Kyela.
Sifa za Wanyakyusa wa Kyela
1. Wengi si wapole mtu afanyapo kosa
2. Wacha
Mungu
3. Wanajua kupenda
4. Hawapendi
dharau
5. Wanapenda kujulikana (hasa kama wamesoma hadi kupata
digrii n.k.)
6. Wapiganaji sana kimaisha
7. Wana
wivu katika masuala ya mapenzi
8. Wanapenda
haki itendeke, hawapendi ubabaishaji
9. Ni watu shupavu sana kwenye kazi za kujitolea hasa za kijamii
Sifa za Wanyakyusa wa Tukuyu
1. Wapole
2. Wacha Mungu
3. Wanajua kupenda
4. Hawapendi dharau kabisa
5. Wanajituma kwenye
kazi, hasa kilimo
6. Wana wivu sana
7. Wanapenda haki itendeke na hawapendi ubabaishaji
8. Ni watu jasiri na wasioogopa vitisho
9. Ni welevu


Post a Comment

 
Top