Baada ya Simba kuituluza
Azam kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, leo wametepeta tena
mbele ya Ndanda FC ya Mtwara kwa magoli 2-1.
Azam imepoteza game ya pili mfululizo kwenye ligi ikiwa nje ya
uwanja wao wa Azam Complex. Ndanda baada haijapoteza mechi kwenye uwanja wake
wa Nyumbani tangu kuanza kwa ligi.
Magoli ya Ndanda yamefungwa na Omary Mponda na Raphat Hamisi
huku John Bocco akiifungia Azam goli pekee.
Matokeo hayo yanaendelea kuifanya Azam ibaki na pointi 10 ikiwa
imeshacheza game 6 na kuipa nafasi Simba kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 3.
Matokeo mengine:
Mtibwa Sugar 1-1 Mbao FC
Tanzania Prisons 0-0 Mwadui FC
Ruvu JKT 2-0 Mbeya City
Post a Comment