Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu katibu mkuu wa Riadha Tanzania
(RT), Ombeni Zavallan amesema kwamba mashindano hayo yatashirikisha mikoa yote
ya Tanzania bara na Zanzibari.
Alisema tayari wamevitaarifu vyama vya mikoa kuhusu mashindano hayo
ambayo pia yatashirikisha wanariadha waliopo katika timu ya Taifa inayojiandaa
kwa michezo ya olimpiki mwaka huu.
Kaimu katibu mkuu (RT) Ombeni amesema baada ya kumalizika kwa mashindano
hayo kutafanyika mkutano mkuu wa RT mei 29,2016 jijini Dar es salaam.
Akizungumzia
mkutano huo, Zavalla amesema kwamba mkutano huo mkuu utajadiri taarifa ya fedha
ya mwaka mzima, uchaguzi mkuu utakaofanyika Desemba mwaka huu na mambo mengine
yanayohusu maendeleo katika mchezo huo.
Aidha, Zavalla amesema hatua zote zimekamilika na maandalizi ya michuano
hiyo yanakwenda vizuri haswa ukizingatia kila mkoa umejipanga kikamilifu na
tayari vyama vyote vimeshapata mwaliko tayari kwa mashindano hayo.
Mbali na
michuano hiyo, pia kamati ya mashindano ya Olimpiki yanayotarajiwa kufanyika
Nchini Brazili mwaka huu imethibitisha kushiriki kwa timu ya riadha ya
Wakimbizi ambayo inahusisha jumla ya wanamichezo 43.
Timu hiyo ambayo imejipa jina la ROA ambayo ni Refugees Olimpics
Athletics ambao watakuwa wakichuana na wanariadha wengine kutoka Mataifa
mengine Duniani kwenye mashindano hayo ambayo yataanza kutimua vumbi katikati
ya mwaka huu.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti wa kamati hiyo ya maandalozi Thiomas Back amesema tayari
wameshwasiliana na umoja wa Mataifa UN kuhakikisha timu hiyo inashiriki lengo
likiwa ni kufikisha ujumbe wa matumaini kwa wakimbizi wote Duniani
Post a Comment