Hiki ni kiburi kikubwa ambacho United wameamua kuwaonesha Real
Madrid, ni sawa na kusema United hawataki chochote kile toka kwa Real Madrid
bali wanataka waachane na wachezaji wao.
Dau la £60m ambalo Real Madrid wamelituma kwa Manchester United
kumtaka David De Gea ni kubwa sana haswa kwa nafasi anayocheza David De Gea na
ni wazi hii ilikuja kama bahati.
Lakini huwezi kuamini kwani Manchester United wamesema hapana na
hawako tayari kupokea kiasi hicho cha fedha kwani David De Gea hauzwi kwa kiasi
chochote kile na mpango wao ni abaki klabuni hapo.
Haitakuwa rahisi kwa Real Madrid kukubali kushindwa kwani ni
timu ambayo mara zote imekuwa kama inahitaji mchezaji yoyote yule huwa wanamchukua
hata kwa gharama kiasi gani.
Na David De Gea amekuwa mchezaji ambaye wanamtaka sana na kwa
hakika watarudi tena na ofa mpya ambayo wanahisi inaweza kuishawishi United
kumuuza De Gea.
Post a Comment