PwaniImage copyright
Image captionVisa vya uharamia pwani ya Somalia vimepungua
Maharamia saba kutoka Somalia wamefungwa jela na mahakama nchini Ufaransa baada ya kupatikana na makosa ya kuteka boti na kuua mmiliki wake mwaka 2011.
Maharamia hao wamehukumiwa vifungo vya kati ya miaka sita na 15 jela.
Waliteka boti la Christian na Evelyne Colombo kwenye Ghuba ya Aden.
Wawili hao walikuwa kwenye safari ya kutalii dunia.
Christian aliuawa na mwili wake kutupwa baharini, naye mkewe akashikiliwa mateka kwa saa 48 kabla ya kuokolewa na wanajeshi wa Uhispania.
Maharamia wawili waliotambuliwa kama Farhan Abdisalamn Hassan na Ahmed Abdullahi Akid, na ambao walidaiwa kuhusika katika kuwatafuta na kuwapa kazi maharamia, walifungwa jela miaka 15.
Farhan Mohamoud Abchir, aliyekuwa hajatimiza umwi wa miaka 18 wakati huo na ambaye alianza kuugua ugonjwa wa kuchanganyikiwa kiakili akiwa gerezani kwa mujibu wa wakili wake, amepewa kifungo cha miaka sita jela.
Mwendesha mashtaka alikuwa amependekeza wafungwe miaka 22.
EU
Image captionWanajeshi wa EU walitumwa kukabiliana na maharamia
Christian na Evelyne walkuwa wameuza mali yao yote kabla ya kuanza safari hiyo.
Waliondoka bandari ya Aden nchini Yemen mapema Septemba 2011 wakielekea Oman boti yao ilipovamiwa na maharamia hao.
Visa vya uharamia vilipungua sana pwani ya Somalia hasa baada ya majeshi ya Ulaya kuingilia kati.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, hakuna meli yoyote kubwa iliyotekwa ikilinganishwa na meli 47 zilizotekwa mwaka 2010, visa vilipokuwa juu zaidi.

Post a Comment

 
Top